Pages

Monday, October 1, 2012

Lady Gaga bado anang'ara na vazi la nyama uko tayari kukutana na mwimbaji mwenye vituko lukuki lady Gaga ndani ya vazi lake la nyama ya ng'ombe?Mwimbaji huyu nyota bado anaonekana kutoacha tabia yake ya kuwachajiza watu wasio kula nyama maarufu kama vegetarians kwa rugha ya kimataifa yani'kiinglishi'kwa kulivaa tena vazi lake hili katika shoo huko Amsterdam Uholanzi.

Vazi hili limetengenezwa kwa namna ya ubunifu wa hali ya juu huku likiwa limekaa sambamba na mwili wake kuanzia kwenye mapaja,makalio,mgongoni hadi usawa wa maziwa bila ya kushikizia mabega yake.Mwezi uliopita Gaga alilivaa vazi lake hili kwenye shoo yake ya Budapest na kulirudia tena safari hii njini Amsterdam.

Pamoja na kwamba vazi hili humuonyesha namna Gaga alivyo umbika lakini kali zaidi ilikuwa mnamo mwezi wa tisa mwaka 2010 pale alipopigilia bikini iliyotengenezwa kwa nyama kwenye shoo ya Vogue Japani.Vazi maalumu la nyama lilivaliwa kwenye utoaji wa tuzo za video za muziki lakini sasa limekuwa ni sehemu ya kutokea kwenye sherehe za Rock $ Roll,maonyesho ya Hall of Fame,Women Who Rock na ziara yake ya hivi karibuni Washington DC.

No comments:

Post a Comment