Afrika, ni bara la wanawake au wanaume?

Pamekuwa na mafanikio kadhaa kwa wanawake wa Afrika katika
miezi kumi na miwili iliyopita,
kukiwepo tuzo mbili za Nobel, rais wa pili
mwanamke na mwanamke wa kwanza kuwa mkuu wa Umoja wa Afrika. Kwa mjadala wa
Afrika wa BBC, tunauliza iwapo wanawake wa Afrika wanaongezeka katika ngazi ya
uongozi.
Hata hivyo maswali kadhaa yanapaswa kuulizwa kabla tuseme kuwa wanawake
wanaongezeka kwenye ngazi ya uongozi au la.
Kwanza kabisa ni kipi chanzo cha ukandamizaji kwa wanawake? na je wanaweza
kukabiliana na hili kwa wao kuwa marais wa nchi?Ni kitu gani kinachojumuisha kuingia kwa wanawake uongozini Afrika. Wanawake wa Afrika ni wapi? Na hususan zaidi, wanawake hawa wanaochukua uongozi je ni wawakilishi wa wanawake Afrika?
Utafiti unaonyesha wazi kwamba kiini cha ukubwa wa mwanamume ni chanzo cha ukandamizaji wa wanawake wengi Afrika.
Ili wanawake waweze kuongezeka katika ngazi za uongozi, fikra ya kuwaona wanaume kuwa bora zaidi ni lazima ifutike.
Kutokana na uhusiano huu wa kijinsia, mtu huwaza je mwanamke kuchukuwa uongozi wa taifa hususan ikizingatiwa upendeleo uliopo wa jinsia moja katika taifa lenyewe, kutaleta mabadiliko?

Rasia wa Malawi Joyce Banda
Na kwa hakika ili kudumu katika uongozi huo ni lazima awe na uwezo wa kutekeleza majukumu kama mwanamume na alihakikishie taifa kuwa ataendelea kuwatukuza wanaume.
Suala jingine muhimu kukumbuka ni kuwa hivi sasa ni nchi mbili pekee kati ya 54 Afrika zinaongozwa na wanawake.
Mizani hii iliyoegemea upande mmoja kwa wengine wanaitazama kuashiria kuongezeka kwa wanawake katika uongozi.
Kwa mujibu wa ripoti ya kongamano la uchumi duniani mwaka 2011 pengo la kijinsia linaashiria kuwa nchi kumi kati ya ishirini na moja zilizo na kiwango kikubwa cha ukosefu wa usawa wa kijinsia kati ya wanawake na wanaume zipo Afrika.
No comments:
Post a Comment