Pages

Tuesday, October 2, 2012


Uchaguzi wa Marekani: Vitu 5 muhimu

 
Heka heka za uchaguzi nchini Marekani
 
Jumatano hii mjadala wa kwanza wa kampeini za uchaguzi wa urais nchini Marekani utafanyika .
Mwezi mmoja kabla ya siku ya uchaguzi Novemba tarehe sita, haya hapa mambo matano unayopaswa kuyafahamu kuhusu mchakato wa uchaguzi huo.
 
1. Kuna swala moja muhimu
Takriban asilimia 80 ya wapiga kura wanahisi kama uchumi wa nchi ni swala nyeti na mojawapo ya mambo yatakayowashawishi namna ya kupiga kura. Kulingana na utafiti uliochapishwa wiki jana na kampuni ya utafiti ya Rasmussen .

Swala nyeti zaidi ni uchumi na ajira kwa upande mwingine. Marais waliohudumu muhula mmoja, Jimmy Carter na George Bush Sr waliondoka katika ikulu, wakati nchi hiyo inakabiliwa na hali mbaya na kiuchumi

Ukosefu wa ajira umesalia kuwa juu kwa kiwango cha asilimia 8 kwa miezi 43 na madeni ya nchi hiyo yamepita dola trilioni 16 na hata kuwaacha watu wakijikuna vichwa kujiuliza kwa nini Rais Obama hayuko nyuma kwa kura za maoni au hata kuhoji ikiwa uchumi ni swala nyeti kwa wapiga kura kama wanavyosema wapiga kura wenyewe.

Watu wengi wanahsi kuwa Rais Obama hajafanya vyema katika kura za maoni lakini pia wanahoji ikiwa Romney ataleta mabadiliko yoyote. Na pia idadi kubwa ya wamarekani wanamlaumu Rais wa zamani George W Bush kwa masaibu yao ya uchumi.

2. Ni majimbo machache tu yenye umuhimu.
Uchaguzi huu utategemea sana kura za kubahatisha au majimbo machache kwa sababu sehemu kubwa za nchi hii upande mmoja kuna wanademokrat na mwingine wanarepublican. Sidhani kama hilo litabadilika kwa hali yoyote.
Kila jimbo linapewa idadi ya wajumbe wanaoweza kupiga kura kumchagua rais kulingana na idadi ya watu katika jimbo hilo.
.
Majimbo muhimu kumi : Florida (wajumbe 29 ), Pennsylvania (wajumbe 20), Ohio (wajumbe 18), N Carolina (wajumbe 15), Virginia (wajumbe 13), Wisconsin (wajumbe 10), Colorado (wajumbe 9), Iowa (wajumbe 6), Nevada (wajumbe 6), New Hampshire (wajumbe 4)..Pindi mgombea anapopata kura 270 unashinda urais.

"Uchaguzi uliopita nilikuwa katika jimbo la Indiana. Kinachoudhi sana ni simu unazopigiwa lakini kinacho furahisha ni kuwa watu wamepata mwamko mpya na wanajihusisha na mjadala wa kisiasa."
Kumejitokeza taswira mbili za nchi ya Marekani wakati wa kampeini hizi, moja ambayo huwezi kukwepa matangazo mazito ya kibiashara kuhusiana na kampeini za uchaguzi, na ya pili le ambayo maisha yanaendelea tu kama kawaida kana kwamba watu hawana habari na uchaguzi.

3. Wapiga kura wanabadilika.
Kila mwezi wapiga kura wa Hispania wanaosajiliwa huongezeka hadi watu laki tano nchini Marekani. Jamii ya wahispania ilipita watu milioni hamsini mwaka 2010 ambao sasa ni asilimia kumi na tatu ya watu wote nchini humo.

Mnamo mwaka 2008, rais Obama alipokea asilimia 68 ya kura kutoka kwa walatino.Na huenda akapokea idadi hiyo mwaka huu, kulingana na mtaalamu wa siasa za Latino katika chuo kikuu cha New Mexico, Gabriel Sanchez.
 
"Hoja sio eti Romney ataweza kupokea kura za jamii ya walatino, bali ikiwa idadi ya walatino watakaojitokeza kupiga kura itamwezesha Rais Obama kushinda." Tathmini hii ni pamoja na ikizingatiwa kuwa msimamo mkali wa Romney kuhusu uhamiaji utamnyima kura za walatino.
Mwanasiasa wa Repubican Jeb Bush ametoa wito kwa Romney kulegeza msimamo huo wakati akigusia maswala yanayozua hisia kama vile uhamiahiaji hasa miongoni mwa Latino na wahispania.
Seneta Lindsey Graham amesema waziwazi kuwa idadi ya wazungu wenye ghadhabu, haijatosha kiasi cha kusalia kwenye biashara kwa muda mrefu"

4. Sio tu kuhusu Marekani
Taarifa kuhusu Iran zilizotolewa na wagombea hao wawili:
Obama: "Marekani inataka kusuluhisha mzozo huu kuhusu mradi tata wa Nuklia wa Iran kwa njia za kidiploamsia na tunaamini kuwa bado kuna muda wa kufanya hivyo, lahiki lazima tuwe na kikomo."
Romney: "Tunapaswa kuchukua hatua zozote kuilazimisha iran kusitisha mradi wake wa nuklia."


Wagombea wa uchaguzi wa Marekani Barack Obama na Mit Romney
 
 
5. Yeyote atakayeshinda, tarajia vuta ni kuvute zaidi!
Sio uchaguzi wa urais pekee utafanyika tarehe sita mwezi Novemba. Viti vyote katika bunge la waakilishi pamoja na thuluthi moja ya viti vya bunge la Senate vitawaniwa.
Wakati kinyang'anyiro cha viti hivi hakijaangaziwa sana, huenda umuhimu wake ukaathiri nafasi ya ushindi wa Rais Obama au Mit Romney.

 
 
Chama cha Republican kinadhibiti bunge la wawakilishi huku Democrats wakidhibiti bunge la Senate, pande zote zimekuwa na misimamo mikali kwenye mabunge hayo, mvutano ukaendelea, na hivyo miswaada michache ikapitishwa mwaka 2011,na hivyo likaitwa bunge la kuzembea.

Dhana inayoangaziwa na kufeli kwa mwaka jana kwa kukosa kuafikia makubaliano kuhusu kumaliza madeni yanayokabili nchi hiyo, imesababisha watu kutokuwa na imani na bunge la Congress.
Lakini Rais wa zamani Bill Clinton, alielezea kuwa na matumaini kuwa anataraja bunge la congress kuwa na ushirikiano zaidi baada ya uchaguzi.
Nini maoni yako kuhusu uchaguzi unaokuja wa Marekani?

No comments:

Post a Comment